Kutoka kwa Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa kijana mdogo ndani ya nyumba ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na mkono wangu ulikuwa ukizunguka huku na kule katika sahani (ya chakula), akasema kuniambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kile kinachokuelekea" Ulibakia kuwa ndio ulaji wangu huo hata baada yake. Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-, huyu ni mtoto wa mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ummu Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na alikuwa chini ya malezi yake na usimamizi wake, kwamba yeye alikuwa wakati wa kula akihamisha mkono wake katika pande zote za chombo ili achukue chakula, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamfundisha adabu tatu miongoni mwa adabu za kula. Adabu ya kwanza: Kusema: "Bismillah" Mwanzo wa kula. Ya pili: Kula kwa mkono wa kulia. Ya tatu: Kula upande ulio karibu naye katika chakula.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katika adabu za kula na kunywa ni kusema Bismillahi mwanzo wake.
  • Kuwafundisha adabu watoto, hasa hasa wale walio chini ya malezi ya mtu.
  • Upole wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ameuonyesha katika kuwafundisha watoto na kuwaadabisha.
  • Katika adabu za chakula ni mtu kula kile kinachomuelekea, isipokuwa chakula kikiwa na aina tofauti tofauti, hapo anaruhusiwa kuchukua.
  • Masahaba kushikamana na yale aliyowaadabisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hili tunajifunza kutoka katika kauli ya Omari: Uliendelea kuwa ndio ulaji wangu hata baada yake.