Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mmoja wetu anatokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo, akasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi". Sahihi - Imepokelewa na Abu Daud na Nasai katika Alkubraa
explain-icon

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hutokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo. Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga Takbira mara mbili na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudisha vitimbi vya shetani na kuvigeuza kuwa ni wasiwasi,

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumewekwa wazi kuwa Shetani humuwinda muislamu kwa njia ya wasiwasi; ili kumtoa katika imani na kumuingiza katika ukafiri.
  • Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, kwani Shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
  • Muumini anapasa kuupinga wasiwasi utokanao na shetani na kuuzuia wasiwasi huo.
  • Ni sheria kuleta Takbira kwenye jambo zuri au lenye kufanana na mambo mazuri.
  • Ni katika sheria muislamu kumuuliza mtu mjuzi kwa kila jambo linalomtatiza.