Anasimulia Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa watu wanasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka" [Maaida: 105] Na wanaielewa kuwa mtu anatakiwa ajitume kuirekebisha nafsi yake pekee, na kwamba hatodhurika baada ya hapo kwa upotofu wa wale waliopotea, na kuwa hawajaamrishwa kuamrisha mema na kukataza maovu! Basi akawajulisha kuwa haikuwa hivyo, na kwamba alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Iwapo watu watamuona dhalimu na wasimzuie na dhulma yake, na hali yakuwa wana uwezo wa kumzuia, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kueneza adhabu kutoka kwake kwa wote, anayefanya uovu na anayenyamaza juu yake.