Anasimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi ya kwamba mja anapofanya dhambi kisha akasema: Ewe Mola wangu nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu husema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi hakika nimemsamehe. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi langu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu, afanye atakavyo madamu kila anapofanya dhambi analiacha na anajuta na anaazimia kutolirudia dhambi hilo mara nyingine, madamu ataendelea kufanya hivi, anatenda dhambi na anatubia nitaendelea kumsamehe, kwani toba hubomoa yaliyo kabla yake.