Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.