explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Adhkari (Dua) hatopata hasara wala kujuta msemaji wake, bali maneno haya yanathawabu, na yanakuja kwa kufuatana, na husemwa baada ya swala za faradhi, nayo ni: "Sub-haana llaah" -Ametakasika Mwenyezi Mungu- mara thelathini na tatu, yaani ametakasika Mtukufu na kila mapungufu. "Na Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu, nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Allaahu Akbaru" Mara thelathini na nne, Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno na ni Mtukufu na Mwenye nguvu kuliko kila kitu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Fadhila za kusema Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Allaahu Akbar, maneno haya ndio mema yenye kubakia.