Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema baada ya kumalizika kwa swala za faradhi: Mara thelathini na tatu (33): (Sub-haanallaah) Nako ni kumtakasa Mwenyezi Mungu dhidi ya mapungufu. Na mara thelathini na tatu (33): (Alhamdulillaah) Nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa kamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. Na mara thelathini na tatu (33): (Allaahu Akbar) Nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkuu na Mtukufu kuliko kila kitu. Na kwa kukamilisha idadi ya mia moja (100) "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku, walahul hamdu, wahuwa alaa kulli shai in-Qadiir" Na maana yake: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu ndiye alipwekeka kwa Ufalme kamilifu, na ndiye mwenye kustahiki kutukuzwa na sifa pamoja na mapenzi na kukwezwa pasina mwingine, nakuwa Yeye ni muweza hakuna kinachomshinda. Yeyote atakayesema hivyo, dhambi zake zitafutwa na kusamehewa, hata zikiwa nyingi, kama povu jeupe litokalo juu ya bahari inapochafuka na kutibuka.