explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesahau kutekeleza swala ya faradhi mpaka ukatoka wakati wakati wake, basi anatakiwa aende mbio na afanye haraka kuilipa pale anapoikumbuka, amesema Allah katika kitabu chake kitukufu: "Na usimamishe swala kwa ajili ya kunitaja" [Twaha: 14] Simamisha swala zilizosahaulika unapozikumbuka.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Umuhimu swala na kutozembea katika kuitekeleza na kuilipa.
  • Haitakiwi kuichelewesha swala nje ya wakati wake kwa makusudi bila udhuru.
  • Uwajibu wa kulipa swala kwa aliyesahau na aliyesinzia mpaka atakapo amka.
  • Uwajibu wa kulipa swala haraka hata kama ni katika nyakati zilizoharamishwa.