explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Umuhimu wa kuifanya vizuri sala, na kuzileta nguzo zake taratibu na kwa utulivu.
  • Amemsifu mtu asiyetimiza rukuu yake na sijida yake kuwa ni mwizi, ikiwa ni ishara ya kulichukia hilo, na tahadhari juu ya uharamu wake.
  • Uwajibu wa kutimiza rukuu na sijida ndani ya swala na kutulizana ndani yake.