explain-icon

Ufafanuzi

Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Imani huoza katika moyo wa muislamu na inachakaa kama inavyochakaa nguo mpya kwa kutumika muda mrefu; Na kuoza huko ni kwa sababu ya udhaifu katika ibada, au kwa sababu ya kufanya maasi na kuzama kwenye matamanio. Basi anatoa muongozo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tumuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu azifanye kuwa mpya imani zetu, kwa kutekeleza mambo ya wajibu na kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu uimara na kuzifanya kuwa mpya imani katika nyoyo.
  • Imani sahihi ni kauli matendo na itikadi, na imani inazidi kwa kutii, na hupungua kwa kufanya maasi.