Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa umma kabla yake isipokuwa huwa na watu safi na watetezi, na mujahidina wa kweli kutoka katika umma wake wanaofaa kwa ukhalifa (uongozi) baada yake, wanaofuata Sunna zake na kufuata amri yake, kisha baada ya hao watangulizi wema wanakuja watu ambao hawana kheri ndani yake; Wanasema wasiyoyafanya, na wanafanya yale ambayo hawakuamrishwa kuyafanya, na atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ni Muumini, atakayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumini, na hakuna imani hata chembe ya haradali (ulezi) baada yake.