explain-icon

Ufafanuzi

Anatuwekea wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuingia katika Uislamu, Na kuwa mwenye kusilimu na uislamu wake ukawa mzuri na akawa mtakasifu na mkweli, basi hatoadhibiwa kwa makosa aliyoyafanya kabla ya uislamu, Na atakaye fanya uovu akiwa katika uislamu, yaani kwa kuwa mnafiki au akatoka katika dini yake, basi huyo ataadhibiwa kwa aliyoyafanya akiwa bado hajaingia katika uislamu na ataadhibiwa pia kwa yale aliyoyafanya akiwa katika uislamu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Maswahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutilia umuhimu mambo mazito, na hofu yao kwa yale yaliyokuwa kabla ya Uislamu.
  • Mahimizo ya kudumu kwenye Uislamu.
  • Ubora na fadhila za kuingia katika uislamu, na kuingia katika uislamu hufuta matendo mabaya yaliyopita.
  • Mwenye kutoka katika uislamu na mnafiki, atahukumiwa kwa kila kitendo alichokifanya kabla ya kusilimu kwake, na kuhukumiwa kwa dhambi alilofanya kwenye uislamu.