Ana tafsiri Ibn Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Aya hii tukufu kuwa miungu hii ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu- Kuwa watu wa Nuhu waliusiana kuendelea kuiabudu baada ya kuwa amewakataza Nabii wao Nuhu ziwe juu yake sala na salamu- kutomshirikisha Mwenyezi Mungu- kuwa majina hayo asili yake ni majina ya watu wema miongoni mwao, walichupa mipaka ndani yake kwa ushawishi wa Ibilisi kwao mpaka wakatundika picha zao, Basi jambo likakuwa katika picha hizi mpaka yakawa masanamu yanaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu.