Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua", akawakataza watu wasimfanyie mifano wanaoelekezewa chochote katika ibada zake; na hali wao wanajua kuwa kweli Mwenyezi Mungu yeye pekee ndiye muumbaji na mgawaji wa riziki; nakuwa hawa washirika hawajiwezi bali ni mafakiri (wahitaji) hawamiliki jambo lolote, na ameelezea bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa vijiungu kwa maana ya washirika, na akataja mifano ya kuwafanya hivyo, nayo imefichikana (hiyo shirki) kuliko athari (kishindo cha kukanyaga) cha sisimizi juu ya jiwe jeusi katika giza nene la usiku, kisha akataja mifano juu ya hilo: nayo ni mtu kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kubwa zaidi kuliko hilo ni kumsawazisha huyo na Mwenyezi Mungu ukasema: Namuapa Mwenyezi Mungu na maisha yangu, au ukaitazama sababu bila kumjali msababishaji, na wala usilirudishe jambo kwa Mwenyezi Mungu, ukasema: Lau kama si mbwa huyu anayetulinda basi wangetujia wezi, au mtu akasema: laiti isingekuwa bata hapa nyumbani anayetuzindua anapoingia yeyote mgeni basi wezi wangelitujia, na ni katika shirki pia: kauli ya mtu kumwambia mwenzie: akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, na kauli ya mtu: lau kama si Mwenyezi Mungu na fulani, kisha akatilia mkazo juu ya hayo yote kuwa ni shirki ndogo, na ikiwa ataitakidi kuwa mtu au bata au mbwa ndiyo inayoathiri yenyewe bila Mwenyezi Mungu basi hiyo ni shirki kubwa.