Aliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.