Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha), atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama kuwaambia, pindi watu wote watakapolipwa kwa matendo yao: 'Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwao duniani, mtazame je mtapata kwao malipo?". Ni nzuri (Hasan) - Imepokelewa na Ahmad
explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa jambo kubwa zaidi analoliogopea juu ya umma wake: Ni shirki ndogo nayo; ni mtu kufanya kwa ajili ya watu. Kisha akaeleza kuhusu adhabu ya wenye kujionyesha siku ya Kiyama kwa kuambiwa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkifanya kwa ajili yao, mkatazame je wanamiliki malipo na thawabu za kukupeni kwa amali hiyo?!.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ulazima wa kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutahadhari na riyaa.
  • Huruma yake kubwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya umma wake na pupa yake ya kutaka kuwaongoza na kuwapa kwake nasaha.
  • Ikiwa hii ndio hofu yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akizungumza na Masahaba ambao ndio watukufu kwa watu wema, basi hofu kwa wale wataokuja baada yao ni kubwa zaidi.