Alichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.