Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.