explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za Allah na rehema zake, nakuwa muislamu ikiwa ni katika mazoea yake kufanya matendo mema akiwa katika hali ya afya na yuko nyumbani, kisha apatwa na udhuru akaugua akashindwa kutekeleza ibada hizo, au akashughulishwa na safari, au udhuru wowote; basi huandikiwa malipo kamili, kama ambavyo angefanya wakati wa afya na yuko nyumbani.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Upana wa fadhila za Allah kwa waja wake.
  • Himizo la kuongeza juhudi katika ibada na kutumia fursa ya nyakati za afya na wasaa.