Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema: Nimetayarisha na nimeandaa kwa ajili ya kuwatukuza waja wangu wema peponi mambo ambayo uhalisia wake hakuna jicho liliwahi kuona, na wala sikio lolote kusikia wasifu wake, wala kutokea wala kupita ndani ya moyo wa binadamu yeyote uhalisia wake. Akasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Someni mkitaka: "Nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajda: 17]