explain-icon

Ufafanuzi

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Uwovu pamoja na kuwa umekatazwa katika hali zote, katazo hilo linatiwa mkazo katika Hija kwa kuheshimu na kutukuza ibada ya Hija.
  • Mwanadamu huzaliwa pasina kuwa na makosa akiwa kaepukana na madhambi; hivyo hawezi kubeba madhambi ya mwingine.