Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhiwa humo bidhaa kwa kitambaa ambacho kina picha za viumbe hai, ikabadilika rangi ya uso wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akalifunua, na akasema: Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Kiyama ni wale wenye kufanya mfano kwa kutengeneza picha za vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu. Aisha akasema: Tukakifanya kitambaa kile kuwa ni mto mmoja au miwili.