Lilikuja kundi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, walipofika kwake wakasema -kwa kumsifu- kwa baadhi ya maneno ambayo aliyachukia -Rehema na amani ziwe juu yake-, Wakasema: "Wewe ni bwana yetu", Akasema kuwaambia -Rehema na amani ziwe juu yake- "Bwana ni Mwenyezi Mungu" Yeye ndiye mwenye ubwana uliokamilika juu ya viumbe wake nao ni waja wake. Na wakasema: "Wewe ndiye mbora wetu" na mwenye daraja na utukufu wa juu kuliko sisi na mwenye sifa nyingi. Na wewe "Ndiye mtoaji zaidi kuliko sisi" na mwingi wa ukarimu na utukufu na daraja ya juu. Kisha akawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake waseme kauli yao iliyozoeleka na wasijilazimishe kutafuta maneno mengine, na kuwa shetani asiwavute katika kuchupa mipaka na kupitiliza kunakopelekea kuingia katika yale yaliyoharamishwa miongoni mwa shirki na njia zake.