explain-icon

Ufafanuzi

Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwenda Aya zingine mpaka wawe wamekwishajifunza elimu liyopo kwenye hizo Aya kumi, na wanazifanyia kazi, hivyo wakajifunza elimu pamoja na kuifanyia kazi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na pupa yao ya kujifunza Qur'ani.
  • Kujifunza Qur'ani kunakuwa kwa kujifunza na kufanyia kazi yaliyopo ndani yake na kuyafanyia kazi, na siyo kuisoma na kuihifadhi peke yake.
  • Elimu inakuwa kabla ya maneno na vitendo.