Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuomba Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amsomee chochote katika Qur'ani, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi nikusomee na hali yakuwa Qur'ani iliteremshwa juu yako?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninapenda kuisikia kutoka kwa mtu mwingine, akamsomea kutoka katika Suratun-Nisaai, alipofikia kauli yake Mtukufu: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa". Yaani: Itakuwa vipi hali yako na hali ya Umma wako pindi tutakapokuleta kama shahidi juu ya Umma wako yakuwa wewe umewafikishia ujumbe wa Mola wako Mlezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sasa, simama hapo katika kisomo chako, anasema bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake: Nikamgeukia ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi kwa hofu ya tukio hilo, na kwa kuuhurumia Umma wake.