Amemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.