Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekaa itikafu katika kuba (hema) ndani ya msikiti wake kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake wakidhihirisha kisomo chao cha Qur'ani kwa sauti kubwa inayowaudhi baadhi yao. Akafunua pazia la hema, na akamlaumu aliyefanya hivyo na hakupendezwa, na akasema: Nyinyi wote mnazungumza na Mola wenu kwa kusoma kwenu Qur'ani, basi mmoja wenu asimuudhi mwenzake kwa sauti yake katika kusoma kwake, au ndani ya swala yake.