Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu viongozi wanaotaka haki zao kwa watu ikiwemo kusikilizwa na kutiiwa, na wanazuia haki zilizo juu yao; kama kutenda uadilifu na kuwapa watu ngawira na kurejesha mali za dhulma na kufanya usawa, unatuamrisha tufanye nini tukiwa pamoja nao?. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampuuza; kana kwamba kalichukia swali hili, lakini muulizaji akarudia mara ya pili na ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta muulizaji ili amnyamazishe. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akajibu na akasema: Sikilizeni kauli zao, na mtii amri zao; kwani wana yao waliyobebeshwa na kulazimishwa kuyafanya ikiwemo uadilifu na raia kuwapa haki zao, na nyinyi mna yenu mliyobebeshwa kama kutii na kutimiza haki na kusubiri juu ya mabalaa.