Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa malipo ya muislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kulingana na yale anayoyatenda muislamu pamoja na waislamu wenzake; atakayetatua na akafariji na akaondoa, na ampa nafuu muumini ya dhiki na tabu miongoni mwa shida za dunia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kumtatulia tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiyama. Na atakayemfanyia wepesi mwenye hali ngumu na akamrahisishia na akamuondolea ugumu wake, basi naye Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi katika dunia na Akhera. Na atakayemsitiri muislamu, kama akiyaona kwake yale yasiyofaa kudhihirishwa katika mapungufu na kuteleza, basi naye Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anakuwa mwenye kumsaidia mja wake, pale ambapo mja anapokwenda mbio kumsaidia ndugu yake katika masilahi yake ya dunia na Akhera, na msaada unakuwa kwa kumuombea dua, au kwa mwili na mali na mengineyo. Na atakayekwenda kwa ajili kutafuta elimu ya kisheria, akikusudia kupata radhi za Mwenyezi Mugnu Mtukufu; Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kwa elimu hiyo njia ya kuingia pepnoni. Na hawatojikusanya watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu, wakikisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakifundishana baina yao, isipokuwa huwateremkia utulivu na amani, na huwafunika na kuwaenea rehema ya Mwenyezi Mungu, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwasifia kwa wale walio karibu kwake, na inatosha kuwa ni fahari kwa mja kutajwa na Mwenyezi Mungu kwa wale walioko juu. Na yatakayekuwa matendo yake ni pungufu, hayatomuunganisha na watu wenye vyeo kwa ajili ya matendo yao, anatakiwa asibweteke kwa utukufu wa nasaba na ubora wa baba zake, na akafanya uzembe katika amali.