Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.