Hakim bin Hizam alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake mahitaji ya kidunia akampatia, kisha akamuomba mara nyingine akampatia, kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ewe Hakim, hakika mali hii huvutia na hupendwa sana, atakayeipata bila kuomba na akaichukua pasina kujikweza na pupa, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa pupa na tamaa ya nafsi basi hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa kama yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu wenye kutoa ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini unaoomba, anasema Hakim: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, namuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitopunguza mali ya yeyote kwa kumuomba chochote baada yako mpaka niondoke duniani. Basi akawa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Abubakari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuita Hakim ili ampatie sadaka, anakataa kupokea chochote, kisha kiongozi wa Waumini Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alimuita ili ampatie mali, akakataa kuchukua, basi Omari akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi nimemletea haki yake aliyomgawia Mwenyezi Mungu kutoka katika mali ya Ngawira waliyoipata Waislamu kutoka kwa Makafiri pasina vita wala mapigano, akakataa kuichukua, Hakim hakupunguza mali ya yeyote kwa kumuomba baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.