Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watakapoingia watu wa peponi peponi, Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka atasema kuwaambia: Je, mnahitaji chochote nikuongezeeni? Watasema watu wa peponi wote kwa pamoja: Kwani hujazitia nuru nyuso zetu, kwani hujatuingiza peponi, na ukatuokoa na moto? Hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa pazia na kulinyanyua; na pazia lake ni nuru, watajikuta hawajapewa kitu wanachokipenda zaidi kwao kuliko kumtazama Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.