explain-icon

Ufafanuzi

Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Haitakiwi kwa muislamu kumuanza yeyote katika Mayahudi na Wakristo kwa salam, na makafiri wengineo.
  • Inafaa kujibu salam zao wao watakapoanza kutoa salam kwa kusema: Na kwenu pia.
  • Haitakiwi kwa muislamu kukusudia kumuudhi kafiri kwa kumbana kwa makusudi pasina sababu; ili amsukumie mahala pafinyu pa njia; lakini njia ikiwa nyembamba au inamsongamano basi muislamu ndiye mwenye haki zaidi, na kafiri ndiye apishe.
  • Kudhihirisha utukufu wa waislamu na unyonge wa wasiokuwa wao, pasina kuwadhulumu au kuwaambia maneno machafu.
  • Kuwabana makafiri ni kwa sababu ya ukafiri walionao wa kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, huenda hilo likawa sababu ya kusilimu; akasalimika na moto, ikiwa hilo litawafanya kujua sababu ya kufanyiwa hivyo.
  • Hakuna ubaya kwa muislamu kumwambia kafiri mwanzo wa mazungumzo, vipi hali yako?, Umeamkaje? Umeshindaje? Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo; kwa sababu katazo hapa linachukuliwa ni katika salam ya kiislamu.
  • Amesema Attwayibi: Kauli iliyopendekezwa nikuwa mtu wa bida haanzwi kwa salam, na akimsalimia asiyemjua kisha akabaini kuwa si muislamu asema: Nimerudisha salam yangu, kama kumdharau.