Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja akiitwa: Bin Lutbia ya kukusanya Zaka kutoka katika kabila la Bani Suleim, aliporejea Madina akampa mahesabu ya mali aliyokusanya na aliyotumia, akasema bin Lutbia: Hii ndio mali yenu niliyoikusanya kutoka katika Zaka, na mali hii nimepewa zawadi mimi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake kumwambia: Hivi si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako ili uone je utapewa zawadi ikiwa wewe ni mkweli; kwani hakika haki ulizozifanyia kazi ndio sababu ya kupewa kwako zawadi, na kwamba lau ungekaa nyumbani kwako usingezawadiwa chochote, hupaswi kuihalalisha kwakuwa tu imekufikia kwa njia ya zawadi. Kisha akapanda Mimbari rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya kuhutubia huku akiwa na hasira, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni kama mfanya kazi na muajiriwa katika kile ambacho Mwenyezi Mungu kanipa maamuzi ndani yake miongoni mwa Zaka na Ngawira, kisha anakuja kutoka katika kazi yake na anasema: Hii ni yenu na hii ni zawadi yangu nimezawadiwa! Kwa nini asikae nyumbani kwa baba yake na mama yake ili zawadi yake imfuate, Wallah, namuapa Mwenyezi Mungu, hatochukua yeyote chochote katika vile anavyopewa isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kakibeba siku ya Kiyama juu ya shingo yake, ikiwa alichokichukua ni Ngamia mwenye sauti, au Ng'ombe mwenye sauti ya mroromo, au mbuzi mwenye mlio, basi atapiga kelele. Kisha akanyanyua mikono yake kwa kasi mpaka waliokaa wakaona weupe wa kwapa lake, kisha akasema: Shuhudieni kuwa nimefikisha hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kisha Abuu Humaidi Assaaidi akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Kuwa haya ni miongoni mwa mambo ambayo macho yake yaliyashuhudia na masikio yake yakayasikia.