explain-icon

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza Muislamu kuwa abadilishane zawadi na ndugu yake Muislamu, na kuwa zawadi ni miongoni mwa sababu za mapenzi na kuziunganisha nyoyo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ni sunna kutoa zawadi; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha kufanya hivyo.
  • Zawadi ni sababu ya kuleta mapenzi.
  • Inampasa mwanadamu afanye kila ambacho ndani yake kinaleta mapenzi kati yake na watu wengine, sawa sawa iwe ni katika zawadi au kuwa mpole, au katika maneno mazuri au katika ukunjufu wa uso kwa kadiri awezavyo.