explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakapotoa mtu matumizi kwa familia yake, wale anaolazimika kuwahudumia kama mke wake na watoto wake na wengineo huku akijikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa hilo, na akitaraji malipo kwake kwa yale anayowahudumia basi atakuwa na malipo ya sadaka.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hupatikana malipo na thawabu kwa kuihudumia familia.
  • Muumini hutaraji radhi za Allah katika amali yake na yale yaliyoko kwake katika malipo na thawabu.
  • Ni lazima kuhudhurisha nia njema katika kila amali, na katika amali hizo ni wakati wa kuhudumia familia.