Alitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.