explain-icon

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kusafisha meno kwa kijiti cha mti wa Arak na mfano wake husafisha kinywa kutokana na uchafu na harufu mbaya, Nakuwa ni katika sababu za kumridhisha Allah Mtukufu kwa mja; kwa sababu ndani yake kuna kumtii Allah na kuitika amri yake, na pia kuna usafi anaoupenda Allah Mtukufu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa mswaki, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuuhimiza umma wake kukithirisha kupiga
  • Katika mswaki ni bora kutumia kijiti cha mti wa Arak, na kutumia miswaki ya brashi na dawa ya meno hukaa badala yake.