Ameeleza mama wa waumini Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema siku moja: Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyopendezeshewa na Mwenyezi Mungu kwake kuyasema: "Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea" [Baqara: 156], "Ewe Mwenyezi Mungu nilipe" na unipe malipo ya subira yangu "katika msiba wangu", na unipe badala "na unirejeshee" kwa hilo "kheri kuliko hiyo"; isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa mbadala bora kuliko hilo. Akasema: Alipofariki Abuu Salama akasema: Ni nani katika Waislamu atakuwa bora kuliko Abuu Salama?! Nyumba ya kwanza iliyohama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi Mwenyezi Mungu alinisaidia nikaisema kauli hiyo, Mwenyezi Mungu akanipa badala Mtume rehema na amani ziwe juu yake bora zaidi kuliko Abuu Salama.