explain-icon

Ufafanuzi

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atakuwa na Birika siku ya Kiyama urefu wa Birika hilo ni sawa na mwendo wa miguu wa mwezi mzima, na upana wake hivyo hivyo, Na kuwa maji yake ni meupe kulio maziwa, Na kuwa harufu yake ni nzuri kuliko harufu ya Miski, Na Mabirika yake ni mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi wake, Atakaye kunywa katika Mabirika hayo hatopatwa na kiu milele.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Birika la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mkusanyiko mkubwa wa maji wanaokwenda kunywa humo waislamu miongoni mwa watu wa umma wake siku ya kiyama.
  • Kupata neema kwa mwenye kunywa katika Birika na kwa hivyo hatopata kiu milele.