Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kakaa katika kundi la Maswahaba zake, akiwa miongoni mwao Abubakari na Omari, akasimama rehema na amani ziwe juu yake akaondoka, kisha akachelewa, wakahofia asijekupatwa na kero kutoka kwa adui; ima kwa kutekwa au kinginecho. Wakasimama Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakiwa na mfadhaiko, akawa wa mwanzo kufadhaika ni Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake, akaondoka mpaka akafika katika Bustani ya Bani Najjari, akaanza kuizunguka huenda anaweza kupata mlango ulio wazi akawa hakuupata, lakini alipata upenyo mdogo katika ukuta yanapoingilia maji, akaukunja mwili wake mpaka akaingia akamkuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia? Akasema: Ndiyo. Akasema: Umepatwa na nini?. Abuu Huraira akasema: Ulikuwa pamoja nasi, ukasimama ukaondoka na ukachelewa, tukahofia usijekudhurika mbele yetu, nikawa mimi ndio wa mwanzo kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikapenya kama anavyopenya mbweha, na hawa watu wakiwa nyuma yangu. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampa viatu vyake kama nembo na alama kuwa yeye ni mkweli, na akasema kumwambia: Nenda na viatu vyangu hivi, utakayekutana naye nyuma ya ukuta huu, akiwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na wala hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, moyo wake ukiwa na yakini nalo; atakayekuwa na sifa hii basi huyo ni katika watu wa peponi. Akawa wa kwanza kukutana naye ni Omari, akasema kumwambia: Ni vya nini viatu hivi ewe Abuu Huraira? Akasema: Hivi ni viatu vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amenituma kwavyo kwa yeyote nitakayekutana naye akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu moyo wake ukiwa na yakini na hilo, basi nimbashirie Pepo. Omari akapiga kifua cha Abuu Huraira kwa mkono wake akaanguka kwa nyuma, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na mfadhaiko na uso wangu ukiwa umebadilika nikiwa nataka kulia, na Omari akanifuata na akawa anatembea nyuma yangu. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Umekuwaje ewe Abuu Huraira? Nikasema: Nimekutana na Omari, nikamueleza ulichonituma, akanipiga kipigo kikali, nikaanguka kwa nyuma, na akasema: Rudi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Omari, nini kimekupelekea kufanya hivyo? Akasema Omari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimtoe fidia kwa ajili yako baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli ulimtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kwamba atakayekutana na Mwenyezi Mungu huku akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo wake ukiwa na yakini na hilo ampe habari nje ya pepo?. Akasema: Ndiyo. Akasema: Usifanye hivyo, kwani mimi ninahofia watu watabweteka kwa kauli hiyo pekee pasina kufanya matendo, acha wafanye. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Basi waache.