explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni: La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao. La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la unyenyekevu na kutokujikweza kwa watu
  • Ulazima wa kusubiri juu ya msiba na kutolalamika.
  • Matendo haya ni katika ukafiri mdogo, na si kwamba mwenye kufanya sehemu katika sehemu za ukafiri anakuwa kafiri ukafiri unaomtoa mtu katika mila ya Uislamu mpaka umthibitikie ukafiri mkubwa.
  • Uislamu umekataza mambo yote yanayopelekea kutengana baina ya waislamu kama kutukana nasaba na mengineyo.