Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, na watu wakiwa mahali pao pa kulala wanapopumzikia katika vipandwa vyao na mahema yao, akamtuma mtu kwenda kwa watu akawaamrishe wakate vikamba vinavyotundikwa kwa wanyama sawa sawa ziwe zimetokana na kamba ya upinde -kamba ya upinde, au kinginecho kama kengele au kiatu, na hii ni kwa sababu walikuwa wakitundika kwa kuogopa kijicho, wakaamrishwa kuvikata; kwa sababu havizuii kwao chochote, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Allah peke yake asiye na mshirika.