Anaeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema akiwa katika maradhi yake ambayo yalikuwa makali na akafariki ndani yake: Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Wakristo, na aliwafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia, na hii ni kwa kuyajengea au kuswali hapo au kwa kuyaelekea. Kisha akasema radhi za Allah ziwe juu yake: Na lau kama si katazo hilo na tahadhari hiyo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na hofu ya Maswahaba kufanywa kaburi la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo kwa makaburi ya Manabii wao, basi lingedhihirishwa na kunyanyuliwa kaburi lake.