Anaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.