Ametuelekeza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye anapotukataza kitu ni wajibu kwetu kukiepuka bila kubagua, na akituamrisha chochote ni juu yetu kukifanya kwa kadiri tuwezavyo. Kisha akatutahadharisha ili tusijekuwa kama umma zilizotangulia pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao pamoja nakwenda kwao kinyume nao, akawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa aina mbalimbali za maangamivu na adhabu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.