Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.