Ameeleza Ubai bin Kaab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina) alikuwa ni mtu anayeishi mbali kuliko wote kutoka ulipo Msikiti wa Mtume, na ilikuwa haimpiti swala yoyote; bali anahudhuria swala zote pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaambiwa: Lau ungenunua punda wa kumpanda katika giza la usiku, na katika joto la Ardhi wakati wa mchana, akasema: Sipendezwi nyumba yangu kuwa karibu na msikiti, hakika mimi ninataka aniandikie Mwenyezi Mungu hatua zangu wakati wa kuja katika swala msikitini, na kurudi kwangu ninaporudi kwa watu wangu, yakafika maneno yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hakika amekukusanyia Mwenyezi Mungu kwako yote hayo".