Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuliko mapenzi ya mama yake na baba yake na kijana wake wa kuime na wa kike na watu wote, na mapenzi yanaambatana na kumtii na kumtetea, na kuacha kumuasi.