explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu. Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Utiifu humzidishia mja ukaribu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Ni Sunna kukithirisha dua katika sijida; kwani ni katika maeneo ya kujibiwa.